Ndugu
wa aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari
Juhudi, Gongo la Mboto, marehemu Jacqueline Matiko, wakitoka katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam mara baada ya
uchunguzi wa mwili, uliofanyika juzi.
Kulingana
na maelezo ya mmoja wa madaktari kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili
walioufanyia uchunguzi wa kitabibu mwili wa marehemu Jacqueline Matiko,
mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo
Gongo la mboto, amesema ripoti ya madaktari kuhusu uchunguzi wa sababu
za kifo hicho cha kutatanisha itaiwasilishwa polisi kwa ajili ya hatua
zaidi.
Mwanafunzi
huyo alikutwa amekufa maji Januari Mosi mwaka huu katika Hoteli ya
Southern Beach, iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Temeke, Englebert Kiyondo, alikiri kukutwa kwa mwili wa
mwanafunzi huyo na kwamba kutokana na madai ya ndugu zake, mwili huo
umefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na jeshi lake
linasubiri ripoti ya madaktari.
Utata
huo unatokana na ndugu wa marehemu ambao walikuwa nao siku ya tukio,
kupingana na maelezo ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwa marehemu alifia
katika bwawa la kuogelea na inadaiwa siku ya tukio marehemu alipotea
katika mzingira ya kutatanisha akiwa hotelini hapo, mpaka waliporudi
kesho yake nakukuta mwili wake umefunikwa kwa shuka, pembeni ya bwawa la
kuogelea.
“Inashangaza
wenzangu walikuja wakaambiwa hajaonekana lakini tuliporudi tena
baadaye, bila kutarajiwa tukaukuta mwili. huku askari polisi wakiwa
wameitwa kuja kuuchukua,”Musa Matiko.
Baadhi
ya kinamama ambao walishiriki katika kuosha mwili wa marehemu
mwanafunzi huyo waliliambia Mwananchi kuwa kuna kila dalili kuwa binti
alibakwa kisha kunyongwa kwani shingo yake ilikuwa imevimba na pia
alikuwa na michubuko sehemu za siri.
“Amebakwa
kisha akanyongwa hilo halina ubishi ila tusubiri ripoti za daktari,”
alidai bibi wa mtoto huyo, Saida wakati anatoka katika chumba cha
kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuosha mwili wa
marehemu, ambaye alizikwa katika makaburi ya Gongolamboto, mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Chanzo Mo Blog
No comments:
Post a Comment