Monday, February 11, 2013

WAFANYABIASHARA WALEMAVU WATAKA KATIBA MPYA IWATAMBUE WENYE ULEMAVU



UMOJA wa Wafanyabishara Walemavu Dares Salaam (UWAWADA), umeitaka Katiba Mpya iwe na kipengele kitakachowatambua  watu wenye ulemavu kuwa moja ya sehemu ya watunga sera.

Akizungumza wakati wa mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, kuhusu katiba, Mwenyeki wa Umoja huo, Mohamed Kidumke, alisema kilio chao kutengwa katika maamuzi yanayohusu haki zao ni cha muda.

Alisema anaamini kipengele hicho kitasidia katia ushirikiswaji mipango ya utungaji sera ambazo ndizo zinazosimamia mafanikio ya kila mtu nchini.

Kidumke alisema wanataka ushirikishwaji katika maamuzi ikiwemo katika upatikanaji wa viongozi, kinyume na sasa wamekuwa wakichaguliwa watu ambao hawazijui shida zao.

“Tunataka kilio chetu kifike ngazi ya juu na kitakapo fika huko kifanyiwe kazi na kupatiwa ufumbuzi”alisema Kidumke.

Aliongeza kuwa, jamii ya watu hao ni asilimia 4.5 ya watu wote nchini hata hivyo, bado uwakilishi wake katika vyombo vya maamuzi haupo kabisa kitendo kinachowanyima fursa mbambali za maendeleo.

Naye muwezeshaji, Peter Kiangi aliwataka washiriki wa mafunzo hayo ya Katiba kuyatumia vema kwa kufikisha ujumbe kwa wenzao kwani suala la katiba linagusa maisha ya kila mtu.

Vilele alitoa wito kwa jamii kuacha kuwanyanyapaa watu hao wenye ulemavu kutokana na ukweli kwamba kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.

Awali mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Machinga Compelex, Godwin Mbaga ambaye ni diwani wa Kata ya Upanga Magharibi, alisema katika taifa lolote lile duniani Katiba ni muhimu, msingi wa maendeleo ya maisha ya wananchi wan chi husika.

“Katiba ni sawa na injini ya gari, hivyo tukiwa na gari lenye injini nzurituna uhakika wa kufika safari yetu salama kwa hiyo maoni yenu ni muhimu kwani yatasaidia kupatika katiba itakayolinda maslahi yenu

No comments:

Post a Comment