Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
kwa Kushirikiana na Taasisi ya Wadau wa Nishati Jadidifu Nchini Tanzania
(TAREA) Wameandaa Warsha ambapo wadau mbalimbali wa Nishati
watabadilishana Mawazo juu ya hali halisi ya Tecknolojia Jadidifu
nchini Tanzania.
Katika Warsha hiyo, wadau watatoa maoni
juu ya Mfumo na Mbinu za kukusanya na kuendeleza taarifa kuhusu
maendeleo ya Nishati Jadidifu.
Aidha katika Warsha hiyo COSTECH na
TAREA watabadilishana makubaliano ya Ushirikiano kati yao juu ya Mambo
yote yanayohusu utafiti wa teknolojia ya Nishati Jadidifu.
No comments:
Post a Comment