BARCELONA,
Hispania
Nyota huyo ambaye alirejea kutoka tatizo la majeraha na kumudu kucheza mechi dhidi ya AC Milan ya Italia na Sevilla, na sasa yu shakani kuwahi pambano la marejeano mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Milan hapo Machi 12
KIUNGO wa FC Barcelona, Xavi Hernandez jana alilazimika
kulikosa pambano la mahasimu ‘El Clasico’ dhidi ya Real Madrid lililoisha kwa kikosi cha kulala mabao 2-1 na anatarajia
kuwa nje ya uwanja kwa siku 15 kutokana na kuumia nyama za paja, Barca ilisema
juzi katika taaifa yake.
Xavi nyota wa kimataifa wa Hispania, alirejea tatizo lake la
misuli katika pambano lililoisha kwa kikosi chake kulala nyumbani Nou Camp kwa
mabao 3-1 na kutolewa katika Kombe la Mflame na Madrid – mechi iliyopigwa Jumanne iliyopita.
Nyota huyo ambaye alirejea kutoka tatizo la majeraha na
kumudu kucheza mechi dhidi ya AC Milan ya Italia na Sevilla, na sasa yu shakani
kuwahi pambano la marejeano mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Milan hapo Machi 12.
"Mechi dhidi ya Milan na
Madrid, hatukuwa wazuri kama ilivyo kawaida
yetu, lakini sio sababu ya kutufanya tukate tama dhidi yao," alisema Kocha Msaidizi wa Barca, Jordi
Roura kuviambia vyombo vya habari kuelekea mechi ya jana usiku na ile ya Machi 12.
"Timu inatarajia kupiga hatua na kuwa tayari kushindana
kwa kila kitu. Mtazamao chanya na upiganaji wa aina yake miongoni mwa wachezaji
wetu – unastahili kupongezwa."
Roura, msaidizi wa Tito Vilanova, alikiri kikosi chake
kuumia baada ya kuwaudhi mashabiki wa nyumbani kutokana na kichapo cha katikati
ya wiki, lakini akasema njia bora ya kurejesha amani kwa wafuasi wao ni
‘kushindana na kupata matokeo mazuri.’
SuperSport.com
No comments:
Post a Comment