Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba
ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark,
Johannesburg nchini Afrika Kusini.
1.
Kibanda leo
ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya
kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili
wake, hususan kichwani na usoni.
2.
Upasuaji huo
unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la
madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa
taya lake la kushoto.
3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia
lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao
wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake
ambayo iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa
akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne,
alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye
mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama
aliyofayiwa.
5.
Jana Rais Jakaya
Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini
kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema
Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba
wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Tutaendelea
kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee
kumwombea ili apone haraka.
--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
No comments:
Post a Comment