Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mchuano ulikuwa mkali kweli kweli, lakini hatimaye Uhuru Kenyatta ameibuka mshindi wa kinyang'anyiri hicho kwa asilimia 50.3 ya kura zote zilizopigwa huku Raila Odinga akijipatia asilimia 43.28 ya kura zote
RIPOTI KAMILI.....
MTOTO
wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa
anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda
nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.
Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura 6,173,433
dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa
ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni
291/291.
Jumla
ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura
12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura
zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.
Katika
kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu
akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter
Kenneth mwenye kura 72,786.
Mgombea
wa Alliance for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano
akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National
Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.
Nafasi
ya saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa
Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya
ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina.
No comments:
Post a Comment