. Balozi wa Tanzania Nchini
China, Philip Marmo akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania
mjini Beijing, China, baada ya kuwasili leo Machi 17, 2013, akitokea jimbo la
Sichuan. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya
siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akizungumza, nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Beijing, China, Philip
Marmo (wapili kushoto), baada ya kuwasili leo, Machi 17, 2013 akitokea Sichuan.
Kinana na Ujumbe wa viongozi 14 wa CCM yupo nchini China tangu Machi 11, mwaka
huu, akiwa katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha
China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai na Kulia ni Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mjumbe wa Kamti Kuu
ya CCM, Kadija Aboud.
"KARIBU BEIJING", Balozi wa
Tanzania nchini China, Philip Marmo (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, baada
ya Kinana na ujumbe wake kuwasili akitokea jimbo la Sichuani, leo Machi 17,
2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini china kwa ziara ya siku
kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. (Picha na
Bashir Nkoromo).
Baadhi ya
Watanzania waliopo jijini Beijing, China wakichangamkia kupigapicha na Katibu wa
NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (Katikati) nyumbani
kwa Balozi wa Tanzania nchini China.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi
Beijing, wakilaki Kinana na msafara wake, nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing
China, leo Machi 17, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa
Tanzania wanaosoma Beijing, Daninga .Daniel
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani akiwasalimia baadhi ya
Watanzania wanaoishi Beijing China, baada ya kuwasili na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, nyumbani wa Balozi wa Tanzania nchini China, Philp Marmo,
Machi 17, 2013. Kamani ni miongoni mwa viongozi 14, wa CCM waliopo katika
msafara wa Kinana ambaye yupo nchini China na ujumbe huo kwa ziara ya Kikazi
nchini humo, kufuatia mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China
No comments:
Post a Comment