Mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone
akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki
tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama na kulia ni mwimbaji Bonny Mwaitege. (Picha na Habari
Mseto Blog)
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege
akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki
tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa
maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama.
Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatambulisha baadhi ya
waimbaji watakaoshirika katika tamasha la Pasaka 2013.
Na
Mwandishi Wetu
WAIMBAJI Upendo Nkone na
Boniface Mwaitege wamesema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufikisha
neno la mungu kwa waamini watakaojitokeza siku ya tamasha hilo kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, Nkone alisema inaonekana ana wapenzi wengi zaidi katika
nyimbo za kumtukuza mungu ndio maana wamemchagua kupitia ujumbe mfupi wa simu
za mkononi, hivyo ana deni la kuwalipa siku hiyo.
“Nimepata
furaha kwa waamini kutambua kazi yangu, ndio maana na mimni najihisi nna deni,
na nawaahidi kuimba wimbo mpya siku hiyo ambao “Nimebaki na Yesu” ambao
unachochea ibada kwa waamini,” alisema Nkone.
Nkone
alisema uimbaji wa nyimbo za injili ni mgumu iwapo utafanya vibaya na jamii pia
itakukataa ambako pia waamini wanatakliwa kuisoma biblia na kuielewa sambamba na
kumuomba mungu kwa dhati ya kweli.
Naye Mwaitege alisema
amefurahi kupata bahati ya kuwa mmoja wa wahudumu wa neno la mungu siku hiyo
kwa sababu tamasha la mwaka jana hakupata bahati ya kushiriki kwa sababu
alikuwa safarini nchini Kenya.
“Mwaka jana nilitamani kuimba
pamoja na Rebecca Malope lakini bahati haikuwa yangu, ingawa nimepata bahati ya
kuimba na Sipho Mwakabane ambaye naye anatokea Afrika Kusini kama Malope na
Watanzania wenzangu kama akina John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose Muhando,”
alisema Mwaitege.
Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la Gloria Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’ ambayo itauzwa siku hiyo.
Tamasha hilo ambalo
litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa Aprili 3, Aprili 6
mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7.
Viingilio katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi 10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.
Mgeni rasmi katika tamasha
hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
No comments:
Post a Comment