Semina
elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 iliyokuwa ifanyike
Jumanne (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa imesogezwa mbele
hadi Machi 26 mwaka huu.
Uamuzi wa
kusogeza mbele semina hiyo umetokana na maombi ya wadhamini, Coca-Cola
ambao katika tarehe ya awali watakuwa na shughuli nyingine za kampuni
hiyo.
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi wajumbe kwa usumbufu
wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na semina hiyo kusogezwa mbele.
Hivyo, washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam (TFF) siku moja kabla (Machi 25 mwaka huu).
Washiriki hao
ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na
Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa
Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment