Kamanda Liberatus Sabas, akibeba begani mimea aina ya bangi tayari kwa kuikusanya kwapamoja na kisha kuichoma moto katika operesheni hiyo. |
Hapa akifyeka shamba la bangi |
Bangi iliyowekwa kwenye viroba ikiingizwa katika gari la polisi |
Askari polisi wakiwa kwenye mashamba ilipolimwa
bangi hiyo
bangi hiyo
RPC AONGOZA OPERESHENI HIYO
Na Janeth Mushi,Arusha
JESHI la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
usalama,vimefanikiwa kuteketeza Bangi iliyokuw aimeoteshwa katika
mashamba yanayokadiriwa kuwa na ukubwa wa hekari 150.
Aidha bangi hiyo ilikutwa katika vijiji vya Likamba na Imbibya
vilivyopo Wilayani Arumeru mkoani hapa,katika Operesheni iliyoongozwa
na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Liberatus Sabas,iliyoanza majira ya asubuhi,Machi Mosi mwaka huu.
Mara baada ya kikosi hicho kufika katika kijiji cha Likamba
walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wlaiokuwa na viroba vyenye
bangi,pamoja na kufyeka na kuteteketeza kwa moto bangi iliyokuwa bado
haijavunwa.
Katika vijiji hivyo viroba vingi vya madawa hayo ya kulevya
vilionekana vikiwa vimefichwa katika mashamba ambaye yameoteshwa
mahindi,ambapo wenyeji wa maeneo hayo waliyahama makazi yao kw amuda
na kukimbilia maeneo ya milimani ya jirani.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda Sabas alisema jumla ya viroba
vilivyopatikana ni 32 vyenye uzito tofauti huku watuhumiwa watatu
ambao ni JaluoTendevesi (32) na Tikayo Kilamee (23) wote wawili ni
wakulima na ni wakazi wa kijiji cha Ndevesi wilayani Arumeru pamoja na
Ngwerenya Siraitei (55) Mkulima Mkazi wa Mombo mkoa wa Tanga
walikamatwa.
ACP Sabas alitumia fursa hiyo kuwaomba Wataalamu wa kilimo
kuwatembelea wakazi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwapa elimu ya kilimo
mbadala ili ardhi hiyo waitumie kwa kulima mazao ya chakula na
biashara badala ya kuendelea na kilimo cha madawa hayo yenye madhara
makubwa kwa binadamu.
Alisema kuwa mafanikio hayo ni muendelezo wa ushirikiano mzuri baina
ya jeshi hilo na vyombo vingine vya usalama pamoja na wananchi ambao
kwa kiasi kikubwa wanatoa taarifa zinazohusu uhalifu na wahalifu kwa
jeshi hilo mara kwa mara.
Tangu kuanza kwa mwaka huu kwa kipindi cha mwezi
Januari-Februari,Jeshi hilo limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya
aina ya Mirungi viroba 372 vikiwa vinasafirishwa toka nchi jirani ya
Kenya kuingia nchini na pia madawa ya kulevya aina ya bangi magunia
yapatayo 143 huku kesi za matukio hayo zikiwa zimeshafikishwa katika
vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment