Monday, March 4, 2013

MJUMBE WA UVCCM TAIFA AKUTWA HOTELINI AKIWA AMEFARIKI


 
Picture
Benson Mollel
Aliyekuwa mjumbe  wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ngazi ya Taifa  kupitia mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) amekutwa amefariki dunia ndani ya hoteli ya Lush Garden Bussiness Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na  Jacaranda  mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Tukio hilo lililogusa hisia za wengi  lilitokea  ghafla tarehe 3 /3/2013  majira ya saa 6:oo mchana.

Kabla ya kukutwa na umauti Benson alikuwa mfanyabiashara wa madini mkoani hapa ambapo kifo chake kimehusishwa na masuala ya kisiasa na kibiashara.

Marehemu Mollel aliutwaa ujumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoani Arusha mwaka huu akimrithi mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa sasa, Mrisho Gambo katika uchaguzi uliokuwa na mshikemshike huku akitajwa kuwa kambi ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowasa.

Vyanzo vya habari ndani ya hoteli hiyo vimedai kwamba marehemu alifikia hotalini hapo Machi 2 mwaka muda wa usiku akiongozana na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Nancy, ambapo walichukua chumba nambari 214.

Mmmoja wa walinzi hotelini hapo aliyejimbulika kwa jina la Obeid Mollel kutoka kampuni ya ulinzi ya Victoria Support Services ambayo inaimarisha ulinzi hotelini hapo alisema kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.

Alisema wakati wakiwa hotelini hapo, marehemu aliomba kuegesha gari lake jipya ambalo bado halijapata usajili lenye nambari 4093 GX 110 aina ya Mark II Grande ambapo alikubaliwa na kisha kurejea chumbani na mwanamke huyo ambaye anatajwa kuondoka asubuhi ya siku ya tarehe 3/3/2013.

Majira ya asubuhi, mmoja wa wahudumu hotelini hapo alisema kuwa mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maryam aliwasili hotelini hapo majira ya saa 5:00 na kuomba kupelekwa moja kwa moja chumbani kwa marehemu.

Mhudumu huyo alisema kuwa wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa chumbani hapo, marehemu naye alipiga simu mapokezi na kuomba mwanamke huyo apelekwe chumbani kwake ambapo walitekeleza jukumu hilo.

Mhudumu huyo alisema kuwa walimwona mwanamke huyo akitoka ghafla nje ya hoteli hiyo majira ya saa 6:00 mchana bila kumtambua sura yake ambapo hawakufuatilia chochote kwa kujua kwamba hakuwa na nia mbaya.

“Sisi baada ya kumwelekeza yule dada chumba alichofia marehemu, hatukufuatilia, mlinzi alimwona akitoka tena nje ya geti, wala hakukaa muda mrefu,”alisema mhudumu huyo

Mhudumu huyo aliamua kupiga simu ya chumba alichofia marehemu ili kujua  endapo ataendelea kukodisha chumba hicho ama la, lakini katika simu ya chumba hicho ilikuwa haipokelewi.

Wakati hayo yakiendelea alisimulia kwamba mmoja wa wahudumu ambaye alikuwa akifahamiana na marehemu kwa muda mrefu aliamua kumpigia kupitia simu yake ya mkononi lakini nayo vile vile haikupokelewa.

Baada ya hatua hiyo mhudumu huyo aliamua kupanda ngazi kwenda chumbani kwa marehemu lakini katika hali isiyo ya kawaida alikuta mlango ukiwa wazi na mara alipomwamsha marehemu hakuweza kuamka na ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli na kisha kuviarifu vyombo vya usalama.

Endelea kusoma habari hii kwenye JamiiBlog

No comments:

Post a Comment