Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la
mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu
Athumani Kilamboleo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini
Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya
kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili,atakumbukwa
kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye
aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia
amefundisha nyota wengi wa kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard,
Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa
Stars kutokea Yanga na Pan African
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu
wa Yanga Lawrence Mwalusako katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga
na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013
katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. wengine toka kushoto ni Naibu Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika. Ndugu Adam Malima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam
Mhe Ranmadhani Madabida na kulia ni Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya kuongoza
maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na
baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilamboleo Machi 11, 2013 katika
makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment