picha ya pili ni waandishi wa habari waliokuwa
wanasikiliza sakata hilo leo na chini ni wajumbe kutoka Jukwaa la katiba
wakisikiliza kwa makini sakata hilo
Sakata la kutekwa na kutesa kwa watu mbalimbali sasa limehamia jukwaa la katiba . Jukwaa la katiba Tanzania limeviomba vyombo vya usalama ikiwemo polisi na vyombo vingine kuhakikisha vinalinda usalama wa viongozi wa jukwaa hilo kutokana na kile walichokidai ni kutishiwa maisha kwa viongozi wa jukwaa hilo mnamo ijumaa ya wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo mjumbe wa kamati ya utendaji wa jukwaa hilo bw HEBRON MWAKAGENDA amesema mnamo tarehe 12 ya mwezi nne mwaka huu ofisini kwao kulikuja gari yenye namba T126 CCG yenye watu sita waliokuwa wakiwataka viongozi wa jukwaa hilo waondoke nao bila kujitambulisha majina yao na wanakotoka, jambo ambalo amesema walinzi walifanikiwa kuwazuia huku akisema kitendo hicho kimewapa wasiwasi na kuomba ulinzi kutoka vyombo vya usaklama
Bw mwakagenda kuwa ameongeza kuwa baada ya tukio hilo kutokea jukwaa limetoa taarifa kwa vyombo mbalimbali vya usalama ikiwemo kituo cha polisi mabatini,ofisi ya kamanda wa polisi kinondoni,na pia kumtaarifu ispecta jenerali wa polisi IGP SAID MWEMA.huku akisema jukwaa halitaogopa kufanya kazi yake kutokana na tishio hilo.
Aidha pamoja na hatua hizo walizochukua mjumbe huyo amewawaomba wasamaria wema kutoa taarifa kwao au jeshi la polisi wanapopata taarifa zozote za njama dhidi ya viongozi wa jukwaa au viongozi wengine ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru
Dah! Tanzania, my beautiful country, unaenda wapi? eh MUNGU walinde wanaharakati wote wa Tanzania wawe salama
ReplyDelete