Na Bryceson Mathias, Mhonda Mvomero
WANANCHI
wa Mafuta Kata ya Mhonda Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, bado
wameshikilia Msimamo wao wa kuiadhibu Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa
kuendelea kumpigia Kura Nicholous Mbelwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji chao hata kama atakuwa Gerezani.
Hayo
yalisemwa na baadhi ya wanakijiji waliohojiwa kwa nyakati tofauti
karibuni, wakipinga unyanyasaji wa Mtendaji Kata Emili Mjenja ambaye
alifutilia mbali uamuzi wa wananchi wa kumchagua Mbelwa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa Mwenyekiti, badala ya Waziri Juma (CCM).
Mapema Julai, 2012 wananchi wa Mafuta walimkataa na kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wao Juma
kutokana na tuhuma za Ubadhirifu wa Fedha za michango ya Mradi wa
Zahanati ambao sasa umetelekezwa na hivyo kupingwa na wananchi kuwa
michango yao inachakachuliwa Ki-Itikadi.
Mjumbe
wa Halmashauri ya Kijiji Jafari Seleman alikiri kuwepo mgongano wa
kimaslahi kati ya baadhi ya Viongozi wa Kata na wale wa kijiji dhidi ya
wananchi, ambapo alisema kumekuwa hakuna Ueledi katika taarifa za Mapato
na matumizi ya Michango, na kusababisha migogoro.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mbelwa aliyechaguliwa na wananchi baada ya
kuangushwa Juma aliwalaum viongozi wa Kata akiwatuhumu kuwa wanafanya
mchezo na Masha ya Wananchi ambao wanateseka kuokoa nguvu na Juhudi za
Serikali.
Diwani
wa Kata ya Mhonda Salum Mzugi (CCM) alipoongea na mwandishi wa habari
hizi alisema, anasikitishwa kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara
inayohusu upinzani wa vyama kwa sababu inawacheleweshea wananchi
maendeleo waliyokusudia.
Aidha kumekuwepo na malalamiko ya kiasi cha Jumla ya Shilingi Laki 125, 000/- ambapo Sh. 80,000/-
Elfu zikiwa ni gharama za Matofali 800 (kila moja Sh. 100/-), Sh.
45,000/- michango ya wanakijiji kilichowapelekea Mafuta kumuengua
Uenyekiti wa Serikali Juma toka Julai, 2012.
No comments:
Post a Comment