Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Kata ya
Salasala, Abdallah Mpondela akionesha eneo la wazi la serikali ambalo hutumiwa na
wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali pamoja na shughuli za
kijamii. Eneo hilo kwa sasa limevamiwa na mtu asiyefahamika anayedai kuwa ndie mmiliki
wa kiwanja hicho ambacho kina Ofisi ya
Mtaa na Kata. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WANANCHI wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Salasala wamemtaka
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuingilia
kati mgogoro wa kiwanja cha wazi cha serikali.
Akizungumza jana Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kilimahewa Abdallah Mpondela alisema kuwa kiwanja hicho kimeingia katika
mgogoro na mtu ambaye hafahamiki na kusema ndio mmiliki wa kiwanja hicho kukiwa
kuna ofisi ya Mtaa pamoja na ofisi ya Kata hiyo.
Mpondela alisema kuwa mtu huyo ambaye anasema kiwanja hicho
ni mali yake huku Manispaa ya Kinondoni imejenga ofisi katika eneo hilo ambapo
katika ramani inaonyesha ni mali ya serikali.
Mwenyekiti pamoja na wananchi wamesema kuwa hawataweza
kuachia kiwanja hicho kwenda katika mikono ya mtu mwingine kwa masilahi yake
huku wakinanchi wakikosa eneo hilo linalotumika katika michezo na mikutano
mikubwa.
Mpondela alisema kuwa mtu huyo alifikia kwenda mahakamani
kwa kumshitaki Mwenyekiti wa Mtaa ambapo hajaweza kifika kizimbani kusimama
katika kudai hicho kiwanja kuwa ni mali yake tangu ilipofunguliwa kesi na mtu
huyo.
Wakili wa Kujitegemea wa Kutetea kiwanja hicho upande wa
Mwenyekiti wa Kilimahewa Addo Mwasongwe alisema kuwa atahakikisha kiwanja hicho
kinabaki katika mikono ya wananchi kwa shughuli za kijamii.
Mwasongwe alisema kuwa kazi yake ni kuona haki inatendeka
kwa wananchi wa Kilimahewa kuenndeka kumiliki eneo hilo kutokana na ramani
inavyoonyesha kuwa eneo la wazi la serikali.
No comments:
Post a Comment