Wachezaji wa Barack Young Controllers wakiwa na Afisa wa Shirikisho la soka nchini, Mzee Mshangama baada ya kutua uwanja wa ndege leo asubuhi |
Wakipanda basi lao |
Kocha na wachezaji ndani ya basi tayari kwa safari ya hotelini |
Mtoto wa Rais wa Liberia Robert Alvin Sirleaf (kulia) akiwa na mmoja wa mtu ambaye alikuwa kwenye msafara |
Wakishuka kwenye basi kuingia hotelini |
Wakiwa ndani ya Saphirre court hotel |
TIMU ya Barrack Young Controllers II ya Liberia imetua leo asubuhi huku ikiwa na matumaini kibao ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC.
Naye kocha wa timu hiyo, Robert Lartey, amejigamba kuwa uwezo wa kuifunga Azam FC kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho utakaochezwa jijini Dar es Salaam jumamosi kwani makosa yaliyoigharimu timu amekwisha yafanyia marekebisho
“Mchezo huu ni muhimu kwa timu yangu na naamini nitashinda”, alisema Lartey.
Pia alijigamba
kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji ambao pia wapo timu ya
taifa ya Liberia ya Vijana, akina Ezekiel Doe, Benjamin Gbamy na George
Dauda.
Wachezaji wa
timu hiyo wameonekana kuwa nyuso zao kutokuwa na furaha sijui ni kwa
kutafakari kuwa walipoteza mchezo wa awali wakiwa nyumbani na sasa
wanacheza ugenini.
Young
Controllers imetua leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) saa 2:30 kabla ya muda wa 3.35 asubuhi ambao ulitarajiwa kwa
ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo
inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.
Kocha huyo
amesema hali ya hewa ya Dar es salaam haijatofautiana sana na hali ya
hewa ya Liberia jana amekiri Dar es Salaam kuwa na joto kuzidi Monrovia
Msafara wa
timu hiyo umetuwa na watu 37, wachezaji 21 na unaongozwa na Ofisa
Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto
wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, Samuel Sumo wakati Meneja wa
timu ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.
Wachezaji
waliomo kwenye kikosi hicho ni Abraham Andrew, Alfred Hargraves, Alpha
Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu Wee, Ezekiel Doe, George
Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo, Joseph Broh, Junior
Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince Kennedy,
Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.
No comments:
Post a Comment