Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua
Jambo wakati alipotembelea Mradimpunga wa Umwagiliaji kwenye Bonde la
Mpunga la Jendele kulia Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa waziri
alifanya Ziara ya Wilaya ya Kati Unguja kukutembelea Mradi
Uliofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Picha na
Ali Meja)
Mratibu
wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis
Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia
Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye
Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa
Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Ali Issa Maelezo, Zanzibar
Waziri wa nnchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia
Suluhu Hassan amesema kuna umuhimu
mkubwa kwa wana nchi kuituza na kuindeleza miradi inayo fadhiliwa na Serikali
zotembili na washirika wa maendeleo ili
miradi hiyo indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.
Hayo ameyasema leo huko Jendele wilaya ya kati Mkoa wa
Kusini Unguja wakati alipo fanya ziara
kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo ilio fadhiliwa na TASAF kupitia
Serikali ya muungano Tanzania.
Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wana
nchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwalengo kwamba wananchi hao
waweze kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato jambo ambalo baada ya mradihuo
kukabidhiwa wananchi husuasua na hatimae kufa kituambacho hakifurahishi.
Amesema wana nchi wajifunze kuituza na kuendeleza miradi
hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufahisha wao wenyewe.
“kuiacha miradi ife sivizuri ,muichangie
iliijiwezekujiendesha na huko ndio faida ya miradi hiyo”.alisema Samia.
Aidha Waziri aliwambia wakulima wa bonde la jendele Kinyasini
Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu
kwavile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo uzalishaji ungezeke.
Waziri hoyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni
kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyo tumika katika miradi ilio ombewa
na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi.
Waziri alifurahishwa na juhudi zinazo chukuliwa kwani
kumefikiwa hatua kubwa za kumaendeleo na zinatia moyo kwa matumaini
Waziri alitembelea mradi wa
mpunga wa umwagiliaji maji jendele na mradi wa uzalishaji mbegu za
mpunga kinyasini kisongoni na badae kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL
inayo endeshwa na wizara yakilimo na maliasili na ushirika Zanzibar .
Miradi hiyo kwa TASAF ya awamu ya kwaza Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu
ambapo ziligawiwa sawa sawa kwa unguja na pemba.
Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani
2,500.000.00 ambapo zilitumika kumalizia
mradi wa kwaza unguja na pemba kupitia mifuko mitatu nayo ni mfuko wa Taifa wa
kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa
ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00
Ziara hiyo itaendelea kasha kutembelea idara ya uhamiaji
Zanzibar na malaka ya kitambulisha cha Taifa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment