Saturday, September 22, 2012

MBUNGE WA KIGAMBONI AZINDUA KISIMA KATIKA SHULE YA SEKONDARI CHARAMBE


Mbunge wa  Kigamboni Dk Faustine Ndugulile  akipanda Mti kuashiria utunzaji wa mazingira  katika shule ya Sekondari Charambe  ambapo  alisistiza utunzaji wa Mazingira kwa wanafunzi wa Shule hiyo.

Dk Ndugulile akifunua kitambaa kuashiria kutumika rasmi kwa kisima cha maji  katika shule hiyo baada ya kuchangia kisai cha shilingi 2500,000/=zilizowezesha  kuweka umeme jua katika shule ya sekondari Charambe na kurahisisha huduma ya maji kupatikana.
Kufuatia huduma hiyo walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Charambe waliahidi kuongeza juhudi katika kufundisha na kusoma kwa kuwa hawatakuwa na hofu ya kukosa huduma ya umeme na maji ambayo awalli walieleza kuwa ni kikwazo kwao katika kupata elimu bora pamoja na kuwa hatarini kwa ajili ya magonjwa ya milipuko.
Pia  Dk Ndugulile aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tatu ya shule hiyo alitembelea miradi mbali mbali na kuwatunuku vyeti jumla ya wanafunzi  334 wa kidato cha nne.

Wanafunzi walifurahia kuwa na maji katika shule yao

Katika Sekta ya maabara pia nao wamo, hapa mwanafunzi akimpiga somo mbunge wa kigamboni

No comments:

Post a Comment