Thursday, September 27, 2012

WAFANYABIHASHARA WA MAJI WATAKIWA KUUZA MAJI KWA BEI ELEKEZI YA EWURA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza katika Mkutano wa wadau na wananchi wa jiji la Dar es Salaam wa  kukusanya maoni kuhusu udhibiti wa Huduma za maji zitolewazo na Magari yanayosambaza maji  na visima Binafsi , ambapo amewatahadharisha  wadau wanaofanya bihashara ya maji  kutouza maji yasiyoyasalama na kwa bei isiyo elekezi ya Ewura. Amesema kuwa Ndoo inatakiwa kuuzwa kwa Sh, 20 kwa ndoo ya lita 20.
Kadhalika mkuu wa mkoa amesema kuwa EWURA inapaswa kuwa na makini kusimamia usambazaji wa huduma ya maji kwa ni bihashara Haramu sit u kuuza madawa ya kulevya bali pia kuuza kwa bei ambayo mwananchi wa kawaida hawezi kumudu.
Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Landmark jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkuu wa maji safi na maji Taka EWURA Eng, Mutaekulwa Mutegeki, akisoma risala yake katika mkutano wa wadau na wananchi wa jiji la Dar es Salaam wa  kukusanya maoni kuhusu udhibiti wa Huduma za maji zitolewazo na Magari yanayosambaza maji  na visima Binafsi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment