Friday, October 19, 2012

ILIVYOKUWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NCHINI TANZANIA

Hawa ni baadhi ya Waislamu wakiwa katika maandamano leo Mchana
 Vurugu kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.

Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.

Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya Redio One wananchi wanakimbizana hovyo kukimbia mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuwatawanya waumini waliokuwa wakitoka msikitini.

Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, waumini hao wameweza kutawanywa na hali bado tete huku magari ya jeshi la Polisi yakielekea katika maeneo ya Kinondoni ambapo kunadaiwa kuwa hali si shwari na vurugu kama hizo zinaendelea.

Polisi wakiwa katika Doria

JWTZ nao walikuwepo wakitoa Sapport

Hay ndio magari ya JWTZ

Askari walijipanga vilivyo, hapa wanaonekana wakiwa wamesambaa barabarani kuhakikisha kuwa hakuna maandamano ya Waislamu


Jionee Mwenyewe


Waandamanaji walikuwa na Vipeperushi kama hivi

Wajeda hawa

No comments:

Post a Comment