Wednesday, November 14, 2012

WAMILIKI WA NYUMBA WAKAMATA MANISPAA YA ILALA



KATIKA kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Manispaa ya Ilala imewakamata Wamiliki 136 wa majengo ambao wamejenga bila kufuata sheria na kanuni za kuwa na Maegesho maalumu katika majengo yao.
 
Hali hiyo imetokana na majengo mengi kukosa maegesho hali inayosababisha wafanyakazi wa wanaofika katika majengo hayo kukosa nafasi za kuegeshea mari hali inayowafanya kuacha maeneo ambayo siyo rasmi, kuziba barabara  nakusababisha foleni zisizo za lazima.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, jijini jana, Msemaji wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu alisema watu hao wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu.
 
Alisema wamiliki hao, walikamatwa kutokana na kukiuka sheria inayowaagiza kila anayejenga jengo lazima ahakikishe kuwa anajenga eneo la maegesho ya magari.
 
Tabu alisema baada ya wamiliki hao kukamatwa walitozwa faini yenye thamani ya sh milioni 25 ambapo miongoni mwao kuna waliokaidi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Alisema ili kuboresha operesheni hiyo, Manispaa itatumia sheria na Namba 8, za mitaa ya mwaka 1982 na kanuni ya mwaka 2008, ambazo zitatumiaka katika kusimamia na kuwabana wale wote wanaokwenda kinyume.
 
Akifafanua zaidi, alisema Manispaa hiyo  ilitangaza zabuni ya kumpata wakala atakayesimamia kazi hiyo mara baada ya kukamilia upembuzi yakinifu, ataanza kazi mapema mwaka ujao.
 
Tabu alisema Manispaa hiyo inatoa wito kwa kila anayetarajia kujenga jengo kuwa anahakikisha kuwa anajenga maegesho ambayo yatatumika kwa ajili ya magari tu bila kuchanganya na shughuli nyingine kinyume chake atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment