Tuesday, January 1, 2013

CLOUDS TV NA CLOUDS RADIO SASA KUONEKANA KWENYE KING'AMUZI CHA ZUKU

Kampuni ya Zuku Pay TV, Imekubaliana na Kampuni ya Clouds Media Group kufanya kazi pamoja ambapo Clouds Tv itaonyeshwa katika King'amuzi cha Zuku.

Ushirikiano huo umetangazwa Rasmi hivi karibuni baada ya makubaliano baina ya Kampuni hizo Mbili.

Meneja Mkuu wa Zuku Bw, Fadhili Mwasyeba alisema kuwa, Wateja wa Zuku sasa watafurahia huduma zao kwani kile kilio chao cha kutaka Clouds Tv pamoja na Clouds Fm ionekane katika King'amuzi cha Zuku sasa Kimetatuliwa.

 “Tunafurahia ushirikiano wetu na Clouds Media Group, kwani utatuwezesha kuwapatatia wateja wetu Chanel ya Clouds TV na Clouds FM'', alisema Fadhili.

 Aliongezea, kuwa Lengo  kuu ni kuboresha huduma zao na kuongeza programu za kifahari za Tanzania.

Zuku Pay TV inao mawakala zaidi ya elfu tatu ambao wateja wanaweza kulipia ada ya  Zuku Pay Tv kote nchini. Hii ni kufuatia makubaliano ya ushirkiano na kampuni za Maxmalipo, Selcom, Vodacom na Tigo.

Zaidi ya hapo, Zuku Pay TV sasa wana promosheni ya "Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure". Programu hii ya inayowazawadia wateja, itahitaji wateja wa Zuku kuungananisha wateja  kumi (10) wapya au kuunganisha wateja watano (5) wateja wapya na unashinda televisheni ya inchi 42 na inchi 22.

Televisheni ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Zaidi ya hapo, wanajumuisha chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile Zuku Afrika ambayo huonesha  bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema. Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.

No comments:

Post a Comment