Flavian Matata akiwa katika pozi tofauti.
Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara
kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s
Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao
bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu.
Mwaka jana Desemba, Flaviana alishinda tuzo nyingine ya
uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.
Flaviana kwa ambaye kwa sasa anaishi
na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini
Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania
kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.
Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara
katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita
katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania
ikishiriki kwa mara ya kwanza.
Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavaz
mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao
wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.
Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake,
Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana
alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama
sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya
kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass
Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia
faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo
ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment