Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya,
Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi
ikiwa ni sehemu ya kuchangia maoni ya katiba mpya.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati akitoa maoni yake kwa Viongozi wa Tume ya katiba
mpya, iliyofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni
sehemu ya jukumu la tume hiyo la kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa
maoni ya Katiba mpya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akitoa maoni yake.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya,
Jaji Augustino Ramadhan, wakati Tume hito ikiondoka Ikulu baada ya
kupokea maoni ya Mhe. Makamu leo.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa tume ya Kukusanya maoni
ya Katiba Mpya, baada ya mazungumzo yao ya kupokea maoni yaliyofanyika
leo Januari 23, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
DAR ES SALAAM, Tanzania
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana
na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya
Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja
na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan.
Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya kumruhusu Mheshimiwa
Makamu Wa Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna tume hiyo inavyofanya
kazi na namna zoezi zima la kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja
lilivyofanyika na kisha akaeleza kuwa, tume hiyo inaendelea na zoezi
hilo kwa kukutana na makundi maalum sambamba na mtu mmoja mmoja kufuatia
umuhimu wa hoja ambazo tume inakutana nazo na hivyo kuhitaji
ufafanuzi.
Katika muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia
maoni yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais
kujikita zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa
kiuongozi katika serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume
kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni
sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na
kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.
Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili umesaidia kujenga na
kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na
Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.
Tanzania imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa
mfumo wa serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo
kwa nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi
ambazo ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya
kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu, « alisema.
Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa
Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa
Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu
Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume
hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.
No comments:
Post a Comment