Saturday, January 12, 2013

MEYA AMTAKA MDEE KUHAMIA CCM ASEMA AMEPENDA UTENDAJI KAZI WAKE

Meya wa Manispaa ya Kinondono Mstahiki Yusuph Mwenda(katikati)  akiingia katikati ya Daraja la Mbezi Ndumbwi lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam akiwa anasindikizwa na viongozi wa Kata na Mtaa huo kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Mbezi Ndumbwi Bw, Salustian Kimario na aliye mbele ni Diwani wa Kata ya Mbezi  Juu.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh, Yusuph Mwenda,   amemtaka Mbunge wa Jimbo la Kawe Mh Halima Mdee kujiunga katika Chama Cha Mapiduzi ili waje wafanye kazi kwa pamoja ndani ya Chama hicho.
Ameyasema hayo leo katika mkutano wa Kuzindua Daraja la Mtaa wa Ndumbwi kata ya  Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya amesema kuwa anamkubali sana Mbunge Mdee kwa Utendaji kazi wake kwani ni mchapa kazi mzuri katika Jimbo lake.
“Jamani Viongozi wa Chama jaribuni kumshawishi Mhe, Mbunge wetu  wa jimbo la Kawe Halima Mdee ili arudi kwenye Chama cha Mapinduzi tuungane tufanye kazi kwa pamoja”, amesema Mwenda.
Meya pia amewataka wananchi wa Mbezi Juu  kusimamia  Ujenzi wa Daraja linalojengwa Mbezi Juu Mtaa Ndumbwi na kuhakikisha kuwa linajengwa kwa viwango bora.

No comments:

Post a Comment