Wednesday, January 30, 2013

MKUTANO WA CCM-KIGOMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Kasulu Mjini mkoani Kigoma. Nape akizungumza kwa niaba ya CCM Wakuu wa wilaya chini watakaoshindwa kusimamamia watendaji wa halmashauri wakiwamo wa vijiji ambao wanajiona wao ni miungu watu mbele ya wananchi na kutamka bayana kuwa  huu si muda wa kubembelezana katika kuwatumikia wananchi.

CCM imesema kuwa kutowajibika kikamilifu kwa watendaji na wakuu wengine wa idara kwenye halmashauri nchini kumefanya wananchi kukichukia chama hicho kwa kukosa huduma mbalimbali kutokana na uzembe wa watu wachache na sasa wakati wao umefika.
Wananchi wa Heru Juu wakimsikiliza kwa makini Katibu wa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Nape akihutubia katika Mkutano wake katika Kijiji cha Karunga Kata ya Heru Juu, Wilayani Kasulu.Nape pia alipata fursa ya kuzungumza na wanachuo wa Chuo cha Ualimu Kasulu na hapa Mmoja wa wanachuo hao Amina Mrisho akiuliza swali.
 
Wataalam wa kwaito waliungana na Katibu wa Itikadi na Uenzei wa CCM, Nape Nnauye kuburudika na picha ya chini ni wakali wanne ambao walipata zawadi ya mshiko.
Wakazi wa Kasulu Mjini na vitongoji vyake waliofurika  kumsikiliza Nape Nnauye.


Nape aliungana na wanamuziki wa Katag Sound bendi matata ya mjini Kasulu kucharaza nyuzi za gitaa kutoa burudani.

No comments:

Post a Comment