Mkurugenzi wa TCRA Prof John Nkoma akifafanau jambo kwa waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA |
Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Profesa JONH
NKOMA amesema bei za mwingiliano wa simu nchini zimeshuka kutokana na
mawasiliano kuwa juu na kusababisha watu wengi kushindwa kumudu gharama hizo.
Profesa NKOMA
ameyasema hayo jijini dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu bei za mwingiliano wa simu ambapo amewataka wamiliki wa makamupuni ya
simu kuwa na viwango sawa ili kila mtu
aweze kumudu gharama za matumizi ya simu.
Amesema Bei za kupiga
simu kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda
mwingine nchini Tanzania imeshuka kwa asilimia 66% kutoka shilingi 113 kwa mwaka wa 2004 hadi kufikia shilingi 34.92
kwa mwaka wa 2012.
Profesa NKOMA
amesema bei za mwingiliano wa simu hazipangwi na mamlaka ya mawasiliano
Tanzania bali ushindani katika mitandao ya simu ndio huamua bei na
mamlaka ina kazi ya kudhibiti bei
hizo ili zisiwe kero kwa watumiaji ambao ni watanzania kwa ujumla.
Profesa NKOMA ametoa onyo kwa mitandao yote ya
simu ambayo itayokiuka agizo hilo la mamlaka
hiyo la kupunguza viwango hivyo vya simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine
kwamba watahakikisha sheria inafwatwa na hatua zitachukuliwa kwa watakaokiuka
tamko hilo.
Hata hivyo ameongeza
kuwa bei hizo zitazidi kupungua hadi kufikia hadi shilingi 26.96 kwa mwaka wa 2017.
No comments:
Post a Comment