Friday, January 11, 2013

SEMINA NA KIKAO CHA WAHARIRI PAMOJA NA WAANDISHI WA MICHEZO KUFANYIKA ARUSHA


NA GLADNESS MUSHI FULLSHANGWE-ARUSHA
 SEMINA na kikao cha wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa michezo na burudani  nchini, vinatarajiwa kufanyika April 12 na 13  mwaka huu, katika jiji la  Arusha.
 Semina hiyo, pia itakwenda sambamba na kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine ambapo wanahabari hao watatembelea familia na Kaburi la  Sokoine wilayani Monduli ili kutoa pole.
 Maamuzi ya kufanyika semina hiyo na kikao cha wahariri jijini hapa, yalifikiwa juzi katika kikao baina ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari zamichezo  nchini(TASWA), Juma Pinto na viongozi wa TASWA Arusha katika hoteli ya palace  mjini hapa.
 Akizungumza katika kikao hicho, Pinto alisema TASWA inatarajia kuitisha kikao hicho, Arusha ikiwa ni sehemu ya mipango yake,kukifanya chama hicho kuwa  cha kitaifa zaidi na pia kuongeza uelewa  wa masuala ya michezo kwa wanahabari.
 Pinto  alisema ili kufanikisha semina hiyo, TASWA taifa na Taswa Arusha, wanapaswa kushirikiana katika maandalizi ya kutafuta wadhamini, ambapo  pia watashirikishwa wanahabari toka mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Manyara.
 Wakizungumza katika kikao hicho,  Katibu wa  TASWA Arusha, Mussa Juma na Katibu msaidizi Hamza Kalmera walieleza TASWA Arusha kuwa tayari kuandaa  semina hiyo, ambayo itafanyika siku ya kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri mkuu, Edward Moringe Sokoine pia  kutafanyika tamasha maalum la michezo  mbali mbali.

No comments:

Post a Comment