Katibu
wa umoja wa bajaji Mbeya Bw.Ernest Mwaisango
Umoja wa Vijana waendesha
Pikipiki za magurudumu matatu Mkoani Mbeya umeamua kuzindua mpango wa
kutembelea watoto yatima na kutoa misaada kutokana na faida wanayoipata
baada ya kusaijili umoja wao na kuchana na kutumisha kwenye
maandamano ya kisiasa na kusababisha vurugu Jijini .
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa umoja huo Bw.Idd Ramadhan alisema kuwa umoja huo
umepata faida kubwa ya kuongeza kipato na kuwa na utulivu baada ya
kusajili umoja wao na kuzinduliwa na naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya
ufundi Bw.Philip Mulugo na hivyo kuona sababu ya kusaidia watoto yatima.
Alisema lengo kuu la umoja wao
wenye wanachama zaidi ya 800 ni kuinuana kiuchumi kwa
akuwawezesha vijana kuwa vitega uchumi na kuiondokana na umasiki na
kutumia na wanasiasa wasio na mpango wa kusaidia vijana
ambapo wamekuwa wakiwatumia wakati wakiwahitaji na kisha kuwaacha baada ya
kupata faida wao.
Bw.Ramadhan alisema kuwa kwa
kuanza watakuwa wakitembelea watoto yatima kituo kimoja kila mwisho
wa mwezi kwa kuwapa mahitaji madogo ya nyumbani ambayo wamekuwa
wakiyakosa kwa muda mrefu baada ya kuondokewa na wazazi wao
waliokuwa wanawatagemea .
“sisi ni vijana ambao tumeamua kuwa
wajasiliamali ambapo tumejipanga kwa ajili ya kuinuana kiuchumi
lakini kutokana na faida tunayoipata tumeamua kuwa tutakuwa tunaitumia
kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima katika vituo vilivyopo Mbeya
na tutazindua mpango huu mwishoni mwa mwezi.”alisema.
Aidha Katibu wa umoja
huo Bw.Ernest Mwaisango alisema mbali na kutembelea watoto yatima
wamejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanawakusanya vijana ,wamachinga,wapiga
debe ,waendesha maroli na makundi mengine ya vijana kwa ajili ya
kuwahamasisha kujiunga na kuachana na kutumika katika vurugu
zinazoondoa amani ya Mkoa pasipo sababu.
Alisema kuwa vijana
wanazo nguvu za kutosha kujituma katika shughuli mbali mbali na hivyo
kinachotakiwa kwa serikali ni kuungwa mkono katokana juhudi zao na kisha
kuonesha mpango wao unaoweza kuwasaidia kuwakomboa katika maisha ya
kutumika na kuiingia katika maisha ya uzalishaji mali na kisha
kusaidia wengine wasio jiweza.
Bw.Mwaisango alisema kuwa
wameweka mpango kazi katika umoja wao kwa ajili ya kushirikiana na uongozi wa
serikali hususani Jiji la Mbeya ili waweze kufanikiwa katika
mipango yao inayolenga kubadili kabisa sura ya awali ya vijana wa
Mkoa wa Mbeya ambapo ilionekana kuwa kazi yao ni vurugu
ambapo sasa wataongoza nchini kw akufanya kazi na kutunza amani na
utulivu.
No comments:
Post a Comment