WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,
amesema msimamo wa wizara hiyo bado uko palepale wa kuheshimu mipaka
yamwaka 1954, hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi ulioko Mkoa wa Dar es
Salaam na Pwani.
Hifadhi ya msitu huo iliyoko
katika wilaya za Ilala mkoani Dar es Salaam na Kisarawe, Pwani
ilianzishwa rasmi mwaka 1954 kwa tangazo la serikali Na. 306 la Septemba
24, 1954 ambapo unaainishwa katika usajili katika raman yenye usajili Na. JB. 196 ya mwaka 1954.
Kauli hiyo aliitoa juzi jijini, na waziri huyo, wakati
alipokuwa akizungumza na Fullshangwe kuhusu mgogoro wa Wakazi maeneo ya
Nzasa, Kimwani na Nyeburu na Hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi.
“Kumekuwa na mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wanaoishi katika
maeneo ya Nzasa, Kimwani na Nyeburu na Hifadhi ya msitu huu wa
Kazimzumbwi.
Wananchi wanaoishi katika maeneo haya wanadai kuwa nyumba zao
zilivunjwa na mazao yao kuharibiwa baada zoezi la uhakiki wa mpaka wa
hifadhi hiyo uliofanywa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii”alisema Profesa Tibaijuka.
No comments:
Post a Comment