Friday, January 25, 2013

UNDER THE SAME SUN WAPATA MAFUTA YA KUJIKINGA NA MIONZI YA JUA KWA AJILI YA ALBINO

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea haki za walemavu wa Ngozi Under the Same Sun, Bi, Vicky Ntetema (katikati)akionyesha mafuta maalumu kwa waandishi wa habari yatakayomsaidia Mlemavu wa ngozi(Albino) kujikinga na Mionzi ya jua na kuweka ngozi yake katika hali nzuri. yanajulikana kwa jina la Kilimanjaro Sun Care.  Mwanzo kushoto ni Mkurugenzi mkuu na muasisi wa Shirika hilo nchini Canada na Tanzania Bw, Peter Ash ambaye ndiye aliyeleta Mafuta hayo kutoka nchini Canada.
 Bi Nketema amesema kuwa Tayari wamekwisha jenga Kiwanda cha kutengenezea mafuta hayo kitakachoitwa kwa jina la Local Sunscreen Production Unit(LSPU) ambapo kitakuwa maeneo ya RDTS Kitengo cha KCMC Mkoani  Kilimanjaro.
Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwemo kwenye Mkutano huo

Haya ndiyo mafuta yenyewe sasa ambayo yanaweza kutumiwa na watoto pamoja na watu wazima hayo ni kwa ajili ya watoto.

No comments:

Post a Comment