Tuesday, January 29, 2013

WALIMU WAISTUA TENA SERIKALI YA JK


Rais wa Chama cha walimu Tanzania Bw, Gratian Mukoba akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo jijini Dar es Salaam.
 
Serikali ya Jamuuri ya Muungani wa Tanzania inadaiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 25 zinazotokana na kutolipwa kwa Malimbikizo ya Mishahara na Madeni mengine ya walimu Tanzania.

Kufwatia  Madai hayo chama cha walimu Tanzania(CWT) kimeitaka Serikali Kuhakikisha kuwa Madeni hayo yamelipwa  yote kufikia Machi,2013 ili kuepuka msuguano usio wa lazima kati yake na CWT.

Hayo yamesemwa Leo na Rais wa CWT Bw, Gratian Mukoba, wakiti akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.

Mukoba amezungumzia pia swala la walimu 60,000 wanaostahili kupandishwa madaraja hawajapandishwa na kuitaka serikali kuwapandisha madaraja walimu hao mpaka kufikia machi 2013 kwani Bunge lilishapitisha Fedha za Kupandishia Madaraja walimu kuanzia julai 2012.
Aidha Mukoba amesema kuwa Baraza la Taifa litaitishwa kwa ajili ya Kupata taarifa ya Utekelezaji wa maazimio hayo baada ya Muda huo kupita.

Bw Mukoba Mbele ya Kamera ya Mwandishi wa habari

No comments:

Post a Comment