Wednesday, February 27, 2013
Al-Shabaab yatishia Kenya kabla ya uchaguzi
Al-Shabaab siku ya Jumatano (tarehe 27 Februari) ilitoa tahadhari kwa wapiga kura wa Kenya kabla ya uchaguzi mkuu unaokuja, ikiwatishia na "vita vya kutisha vya muda mrefu".
Kikundi hicho cha wanamgambo kilisema kwamba Kenya ilipata shida pale ilipolitawala eneo linalopakana na kusini ya Somalia, lakini hawakusema ni nani ambaye Kenya wanapaswa kumpigia kura tarehe 4 Machi, AFP iliripoti.
"Kama mtaiweka serikali madarakani, kisha kuwa na utashi wa kuvumilia athari za matendo yake, kwako wewe utabeba uzito wote wa mizigo wake," al-Shabaab ilisema kupitia (Twitter.)
"Mabadiliko ya hali ya kisiasa katika nchi yako yanaweza sasa kuwa na umuhimu kwenye siku njema zijazo; siku zijazo ambazo zitahusisha umwagaji damu kidogo," taarifa hiyo iliendelea. "Kwa sasa mna fursa kufikiria tena na kutathmini tena uchaguzi uliwekwa kwenu na serikali inayoondoka madarakani."
Al-Shabaab ilitoa tahadhari kwamba "itafanya chochote itakachoweza kulinda ardhi yao isingiliwe".
Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) vilianza operesheni kusini ya Somalia mwezi Oktoba 2011 kupambana na al-Shabaab baada ya mfululizo wa mauaji na utekaji nyara ndani ya Kenya. Tangu hapo, KDF imekuwa sehemu ya askari 17,000 wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Hakuna mgombea wa urais aliyependekeza kwamba wangeondoa vikosi Somalia.
Tangu uvamizi wa Kenya, washambuliaji wamepiga mabomu na kurusha maguruneti jijini Nairobi, wakati wanaume wenye silaha wameua maofisa wa usalama na raia kando kando ya mpaka wa Kenya na Somalia.
Mashambulio hayo mara kwa mara yamelaumiwa kufanywa na al-Shabaab au wafuasi wao, ingawaje al-Shabaab haijakiri kuhusika na mauaji hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment