BAADHI
ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi Jijini Mbeya wameyalalamikia
baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji wa bidhaa hizo kwa
kutozingatia usalama wa watumiaji.
Malalamiko
hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina
lake kununua soda aina ya Tonic Water inayotengenezwa na kampuni ya Coka
kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina ya Vodka.
Soda
hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka moja eneo la Simike baada
ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini kabla ya kuifungua ndipo
laipogundua uchafu huo.
Kufuatia
hali hiyo Mwandishi wa stori hii alipewa taarifa na mhusika ambapo
walienda moja kwa moja hadi kiwandani Coka eneo la Iyunga Jijini Mbeya na
kupokelea na Meneja mauzo wa wilaya(Area sales Manager)
Baada
ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea meneja huyo aliwapeleka waandishi kwa
kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema tuwaachie soda hiyo baada
ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.
Walidai
waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa kimaabara katika uchunguzi
utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta sintofaham kwa walalamikaji huku
wakihoji uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu unaonekana.
Aidha
walidaikuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda hiyo walisema mlalamikaji
hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika na tatizo hilo licha ya
kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.
Hali
kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji hivyo hasa wanaotumia
nyakati za usiku muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika
vinywaji.
Hata
hivyo mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka kiwanda cha Coka aliiomba
mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea vinywaji
hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili kunusuru afya za wananchi.
(Picha na habari Mbeya Yetu)
|
No comments:
Post a Comment