Uhalifu na kudhuru kwenye malengo ya kuua watu, hasa yanayowalenga
viongozi wa kidini nchini yanachochewa na watu ambao wameachwa kutumia
kiholela uhuru wa mawasiliano.
Angalabu kuna akaunti za mitandao
ya kijamii, magazeti, redio za dini na madhehebu ya Kikristo na Kiislam
zimelalamikiwa nchini Tanzania kwa kueneza mafunzo na mafundisho yenye
chuki, uhasama na kulipiza kisasi, hata ikibidi kwa kumwaga damu.
Litakuwa
ni jambo la ajabu sana endapo Serikali itakanusha kuwa haifahamu kuhusu
haya, kwa maana itakuwa sawa na kuuaminisha umma kuwa Serikali
haifahamu yanayoendelea (out of touch) kwa wananchi wake, hasa
ikizingatiwa ngazi mbalimbali za uongozi zilizomo katika mfumo wa
uongozi, yaani kuanzia mjumbe wa nyumba kumi kumi na viongozi wa mitaa
wanaofahamu yote yanayoendelea katika maeneo yao hadi ngazi ya juu
kabisa Serikalini.
Ikiwa ndivyo, basi aina ya mfumo wa uongozi
tuliyonayo inabidi kufanyiwa marekebisho ili iwe na macho na masikio
yanayowafikia wananchi.
Serikali haipaswi kuamini kuwa kila raia
wake anao uwezo wa kiakili, hekima na maarifa ya kupima na kupembua
mambo na kauli zenye mwisho mbaya dhidi ya zile zenye madhara, hasa
katika misingi ya siasa, dini/imani, kabila, jinsi/jinsia n.k. kwa
kigezo tu cha kudai haki ambayo inakwapua haki ya mwingine, tena
asiyehusika moja kwa moja.
La, sivyo, basi tuamini hizi kauli si
chochezi na basi hazipaswi kuwepo kwenye kundi la kauli chochezi.
Nadhani kauli hizi hata kwenye “comedy” hazi-qualify. Original videos za
kauli hizo zipo YouTube.
No comments:
Post a Comment