Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti Dkt Julius J. Masaga |
Tatizo la miundombinu ya
maabara, vifaa vya maabara na majengo ya kutosha limetajwa kamachangamoto kubwa
inayoikumba secta ya utafiti Tanzania
jambo linalosababisha kutokufanya vizuri sana
kwa sector hiyo
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na mkurugenzi
mkuu wa Taasisi ya taifa ta utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini (NIMRI) Dkt, JULIUS MASAGA wakati
akifungua semina ya siku tatu inayowahusisha wadau wa maswala ya tafiti na
watafiti yenye lengo la kukuza uelewa na kujikumbusha mambo mbalimbali
yanayohusiana na tafiti
Dkt, MASSAGA amesema pamoja na sector hiyo kuonekana inafanya vizuri
ikiwa ni pamoja na watafiti wengi kuongezeka lakini changamoto bado zipo huku
akitolea mfano kama ukosefu wa rasilimali fedha,
na nyingine kubwa kuwa ni ukosefu wa miundombinu ya majengo na maabara za
kutosha huku akisema maabara zilizopo nchini pia hazina vifaa vya kutosha
Katika semina hiyo MASSAGA amesema lengo kuu la Semina hiyo, ni kuwapa watumishi hao uelewa na mafunzo ya kazi za
maadili na pia kupitia tafiti na pia kuzipa tafiti vibali.
No comments:
Post a Comment