Na Dotto Mwaibale
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki nchini, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini na kuuawa yanayoendelea Zanzibar yanaumiza na kamwe yasipewe nafasi.
Pengo alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji ya Padri Evaristi Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar.
Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika Februari 17, mwaka huu wakati akijiandaa kwenda kuendesha ibada ya Jumapili. Pia amewaomba waumini wa kanisa hilo kuwa wavumilivu na kwamba wasilipize kisasi.
Hata hivyo, Askofu Pengo alilalamikia udhaifu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kile alichodai kuwa vimeshindwa kufanyakazi yake inavyotakiwa.
"Vitendo hivi vinavyoendelea kwa viongozi wa dini kuuawa na kujeruhiwa bila ya kuwa na makosa yoyote iwapo havitadhibitiwa ni hatari kwa mustakabali wa taifa," alisema Pengo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Alisema katika tukio la kwanza alishambuliwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae na kwamba baada ya mauaji vilisambazwa vipeperushi vilivyodhihirisha kwamba kulikuwa na makusudio ya kufanya kitu zaidi.
Pengo alisema tukio la kuuawa kwa Padri Mushi si jambo la dharura kwani vyombo vya usalama vingeweza kulizuia.
"Watu wanasema kikundi cha Uamsho hapo Zanzibar ni cha dini, lakini kama ndicho kinachotoa vipeperushi hivyo nini hatima ya mtu mmoja mmoja," alihoji. Alisema kama yeye amepewa vipeperushi hivyo ni wazi Watanzania wengi watakuwa navyo.
Alidai kuwa yeye si kazi yake kuhakikisha kama kweli wahusika wa jambo hilo ni hao watu wa kundi hilo kwani wenye kujua hilo ni usalama wa taifa.
Pengo alisema kulikuwa na udhaifu mkubwa kwa vyombo vya usalama kushughulikia mambo hayo na kufikia hatua isiyopendeza ya kuuawa kwa padri aliyekuwa akienda kufanyakazi yake ya upadri.
"Padri Mushi hakuuawa akiwa baa wala kugombana na mtu yeyote bali akienda kufanyakazi yake ya upadri na ndivyo ilivyokuwa kwa Padri Ambrose ambaye alishambuliwa akienda kufanyakazi hiyo...inasikitisha kwani hakuwa na kosa," alisema.
Alisema kifo cha Padri Mushi si pigo kwa Wakatoliki bali kwa taifa kwa ujumla kwa sababu iwapo katokea mtu wa imani moja kumshambulia wa imani nyingine hatuwezi kujua ni kitu gani kinaweza kutokea baadaye.
Pengo alivitaka vyombo vya usalama kufanyakazi zake kwa umakini zaidi na kuwa yeye si mtalaamu wa masuala ya usalama lakini wangesoma alama za nyakati jambo hilo lisingeweza kutokea.
Alisema jambo hilo limetokea, lakini rai yake kwa Watanzania na viongozi wa nchi ni kuwa wasiruhusu migogoro hiyo iendelee nchini kwa madai kuwa wanaofanya hivyo ni wahuni kwnai ni jambo la hatari kwa nchi.
Pengo alisema kesho saa 4 asubuhi huko Zanzibar itafanyika ibada ya kumuombea marehemu Mushi na taifa kwa ujumla. Pia Tanzania Bara itafanyika saa 11 jioni na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa.

No comments:
Post a Comment