Tuesday, February 19, 2013

WAJENZI UWANJA WA MARACANA WAGOMA


Matengenezo ya Uwanja wa Maracana yakiendelea

RIO DE JANEIRO, Brazil

WAFANYAKZI ya ujenzi wa Uwanja wa Maracana, jana Jumatatu wameingia katika mgomo na kuitia presha Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia – ambayo kabla ya mgomo huu ilikuwa inakabiliwa na hatari ya kutyomaliza ujenzi wa viwanja kwa wakati.

Wafanyakazi hao wanataka ongezeko la mshahara, vocha ya manunuzi ya unga, bima ya afya binafsi na ile ya familia za wajenzi hao – ambapo mgomo wao huo wa simu moja ni utangulizi na unaweza kuwa wa muda mrefu kuanzia wiki ijayo kama hawatosikilizwa.

Maracana dimba maarufu lililotumika kwa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950, unahitajika kumalizwa hara kuwahi fainali za mwaka huu za Kombe la Mabara, kisha fainali za Kombe la Dunia 2014 – gharama ya marekebisho yake ni dola milioni 458.

Uwanja huo unatarajiwa kufunguliwa kwa pambano la kirafiki baina ya Brazil na England – itakayopigwa hapo Juni 2, kisha mechi ya kwanza ya kimashindano itakuwa ile ya Kombe la Mabara hapo Juni 16 kati ya Mexico na Italia.

…..SuperSport.com…..

No comments:

Post a Comment