Friday, February 15, 2013

LICHA YA ULINZI MKALI WA POLISI JIJINI DAR ES SLAAM, WAFUASI WA SHEKHE PONDA WAANDAMANA

7 Baadhi ya wafuasi wa Shekh Ponda wakiwa wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya maadamano bila kibali cha polisi.
8Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
9 Zoezi la kuwakamata na kuwapeleka polisi watuhumiwa hao likiendelea chini ya ulinzi mkali.
10Magari mbalimbali yakiwa yamebeba askari Polisi yakipita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
11Ulinzi ulikuwa ni mkali sana. Polisi wa Pikipiki wakiwa kazini leo. (Picha zote na FULLSHANGWE BLOG).
***
Na Mwandishi wa Father Kidevu Blog, DSM.
Licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuzuia maandamano ya Waumini wa Dini ya Kiislam, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni Waumini wa Dini hiyo katika maeneo ya Buguruni, Malapa na Kariakoo wamefanya maandamano hayo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi kupitia Vikosi vya Kutulia Ghasia-FFU-limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wamebeba Mabango na Mawe kwenye Mifuko katika Mitaa ya Malapa pamoja na Kariakoo.
Katika tukio hilo Uhuru FM imeshuhudia Maduka mbalimbali yakiwa yamefungwa katika Mitaa ya Kariakoo kutokana na maandamano hayo ya watu wanaodaiwa kuwa Waumini wa Dini ya Kiislam.
Waumini hao wanashinikiza Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka-DPP-kumwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya ya Waislam Shekh PONDA ISA PONDA ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Jana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar e s salaam kupitia kwa Kaimu Kamanda wake AHMED MSANGI lilipiga marufuku kufanyika kwa mandamano hayo kutokana na kutokuwa na kibali cha Polisi

No comments:

Post a Comment