Friday, February 15, 2013

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMKATA MKONO MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO)


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.



Mama Maria Chambanenge mlemavu wa ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika na vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa shirika la under the same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo basi uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo.

Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment