Mangula akiteremka katika ndege.
Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Mangula akisalimiana na Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula akisalimiana
na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege Mjini Kigoma
hii leo.
Makamu
Mwenyekiti wa UWT, Dogo Mabruk (kushoto) na Mjumbe wa NEC-Wilaya ya
Uvinza, Asha Baraka pamoja na wanachama wengine wa CCM wakimsikiliza
Mangula.
Vijana wa CCM waliofika kumpokea Makamu Mwenyekiti CCM Bara.
Na Mroki Mroki, FK BLG Kigoma
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula
amewasili mkoani Kigoma asubuhi hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) na kupongeza mabadiliko makubwa yaliyopo mkoani humo
hasa Uwanja huo wa Ndege ambao unaonekana sasa kuwa wa kisasa.
Mangula
ambaye amepata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nappe Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama
hicho ambaye ni Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu. Issa Machibya pamoja na
viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Mangula
amesema Kigoma ya sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi
wanastahili pongezi kwa maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.
“Kigoma
ya leo sio Kigoma ile ya zamani ..uwanja huu wakati ndege inataka kutua
nilitaraji nitasikia matairi ya kihangaika lakini nikashangaa
tunakwenda vizuri tu” alisema Mangula akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.
Aidha
amewaambia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na
mafanikio makubwa yaliyofikiwa hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa
kigoma ambao zamani haukuwa na tabaka la lami ambapo sasa uwanja huo
umewekewa tabaka la lami na kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata zamani
wananchi wa Kigoma.
Pia
Mangula amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli
zinazoendelea kutolewa na wanasiasa wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma
umesahaurika kitu ambacho amesema hakina ukweli kwani mkoa huo sasa
umefunguka kwa miundombinu ya barabara.
Wakati
huo huo, katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha
mapinduzi ccm, mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa
kuwasili kesho mkoani hapa kwa ajili ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa
kufanyika Jumapili Februari 3, 2013 katika uwanja wa Michezo wa Lake
Tanganyika mjini Kigoma.
Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia
zaidi ya themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na
wajumbe wa NEC na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua
maandalizi hayo jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment