Mshambuliaji Wayne Rooney akishangilia moja ya mabao yake akiwa na
wachezaji wa Manchester United walipoichapa Southampron mabao 2-1 juzi
usiku.
Rooney akichuana na mlinda mlango wa Southampton wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Old Trafford.
MANCHESTER,
England
Mshambuliaji huyo sasa ameandika historia mpya ya kufunga
mabao 101 kwenye Uwanja wa Old Trafford akiwa na United – ambayo nayo imekuwa
klabu ya kwanza kushinda mechi 300 za Ligi Kuu kwenye dimba hilo la nyumbani
MABAO mawili aliyofunga mshambuliaji Wayne Rooney katika
kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Manchester
United na Southampton, licha ya kuipaisha zaidi United katika kilele cha Ligi Kuu,
yameweka rekodi mbili za kuvutia kwa nyota huyo na klabu yake.
Mshambuliaji huyo sasa ameandika historia mpya ya kufunga
jumla ya mabao 101 kwenye Uwanja wa Old Trafford akiwa na United – ambayo nayo
imekuwa klabu ya kwanza kushinda mechi 300 za Ligi Kuu kwenye dimba la
nyumbani.
Ni ushindi uliowasukuma juu kwa pointi saba zaidi, lakini
bosi wa United Sir Alex Ferguson alidai: “Tulikuwa na bahati kushinda mechi
hii, lakini pia kushinda ni jina la mchezo hasa katika kipindi hiki cha msimu.
“Katika uzoefu wangu wakati unapokuwa kwenye mchuano wa
ubingwa kunatokea mechi ambazo unakubaliana na ukweli kuwa ulihitaji bahati
kidogo kushinda – na nadhani huu ulikuwa mmoja wa usiku wa aina hiyo.”
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu ya England zilizopigwa juzi usiku, Washika Bunduki
wa jiji la London, Arsenal walitoka nyuma kwa
mabao 2-0 na kumaliza pambano kwa sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool.
Everton waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya West Brom, huku
Norwich City ikitoka sare ya bao 1-1
naTottenham. Fulham wakaiduwaza West Ham kwa mabao 3-1, huku Reading
ikiikaba koo Chelsea
na kutoka nayo sare ya mabao 2-2.
…….The Sun……
No comments:
Post a Comment