Saturday, February 9, 2013

MAOFISA HABARI WA SERIKALI WAMALIZA KIKAO CHAO DODOMA, WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI UPANDAJI WA MITI UDOM

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Raphael Hokororo akiwafundisha Maofisa Habari na Mawasiliano  wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma, Mikoa na Wilaya upigaji wa picha bora  za mnato kwa  matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maofisa hao mjini Dodoma. (Picha Zote na Aron Msigwa - Idara ya Habari MAELEZO)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, akiongea na maofisa hao mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha Maofisa Habari wa Serikali katika Kampasi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM).
 Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

No comments:

Post a Comment