Askofu Laiser siku za mwisho za uhai wake. Hapa alikuwa hospitali ya
rufaa ya Seliani iliyopo jijini Arusha ambako alikuwa amelazwa kwa siku
kadhaa akipata matibabu. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,
akimjulia hali. (Picha kwa Hisani ya JamiiForum.com)
Marehemu Thomas Laiser enzi za uhai wake
Aliyekuwa
Askofu Mkuu wa KKKT Kanda ya Dayosisi ya Kaskazini, Thomas Laizer
(kulia) enzi za uhai wake akitekeleza majukumu yake. Hapa alikuwa
anauombea mwili wa aliyekuwa muhasisi wa chama
cha NCCR Mageuzi katika ibada ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la
OLigilai. (Picha kwa Hisani ya Libeneke la Kaskazini Blog)
Marehemu Askofu Thomas Laiser
ARUSHA, Tanzania
Waumini na Washirika wa Kanisa
Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki
watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia
Alhamisi Februari 14, alasiri
MAZISHI ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Marehemu Askofu Thomas Laizer, yanatarajiwa
kufanyika Ijumaa Februari 15, 2013.
Kwa Mujibu wa Taarifa maalum iliyotolewa na Kamati ya
Mazishi ya KKKT na familia ya Laiser, inasema kuwa, marehemu atazikwa katika
eneo la Kanisa Kuu Mjini Kati, Arusha.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Waumini na Washirika wa Kanisa
Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki
watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia
Alhamisi Februari 14, alasiri.
Pia, taarifa hiyo ya kamati/familia iliongeza kuwa, mwili
wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya mazishi.
Marehemu Laizer alizaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha
Kitumbeni mkoani Arusha na kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane katika
shule ya Longido, alikkomaliza mwaka 1965.
Marehemu wakati wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji
katika makinisa mbalimbali nchini na baade kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi,
kabla ya kutawazwa kuwa Rais wa sinodi na kisha kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa
Kwanza wa Dayosisi ya Arusha, (sasa Dayosisi ya Kaskazini Kati).
Bwana
alitoa, bwana ametwaa, jina lake
lihimidiwe. Ameen.
No comments:
Post a Comment