Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika
kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya
kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha
kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo
Serikali haitachukua hatua.
Mchungaji huyo alifanyiwa
udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika
hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa
kwa kwenda kinyume na mila na destruri ya kuwatahiri kimila, na hivyo
kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.
Mchungaji huyo
anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa
akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana
hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa
vitisho.
No comments:
Post a Comment