Ingawaje si kweli kuwa walioharibika kwa uraibu wa dawa za kulevya
wanaweza kuwekwa kwenye kundi lenye tishio kubwa la kuweza kuutoa uhai
wa wanadamu wengine, lakini kila linapotokea tukio moja tayari ni
takwimu ambayo inafaaa kurekodiwa, kuchunguwa na kisha kujumuishwa na
matukio mengine ili kupata vidokezo muhimu vya jinsi ya kujilinda na
kukabiliana na athari hizo. Kila tukio lina mafunzo! Shughuli ipo katika
kujifunza kutokana na makosa.
Hivi karibuni, wiki iliyopita,
kijana mmoja wa makamo Gift Godlisten Makundi huko nyumbani kwao
Komakundi, Marangu-Mamba, Kilimanjaro ameripotiwa kukatiza uhai wa mama
yake mzazi, Julitha Godlisten Makundi (57) baada ya kumvamia kwa panga
na kisha kumkata kichwa na kukitenganisha na kiwiliwili.
Miili ya
marehemu wote ilizikwa na Mchungaji E. J. Mamkwe wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Komakundi, jimbo la Kilimanjaro
Mashariki katika Dayosisi ya Kaskazini.
Inaripotiwa na mwanamke
aliyefika nyumbani kwa marehemu kushuhudia yaliyotokea, Bi.
Angela-Stella W. Temba kuwa kijana aliyesababisha mauaji alikuwa
akitumia dawa za kulevya na baadaye kurukwa na akili.
Kwamba,
kutokana na matendo yake, mara kadhaa majirani waliwaasa wazazi wake
wammfikishe kituo cha polisi, lakini wazazi hawakufanya hivyo. Hatimaye
wiki iliopita majira ya saa 9 alasiri siku ya tukio, kijana huyo
aliuliza aliko baba yake, ambapo marehemu mama yake alimfahamisha kuwa,
ametoka.
Kwamba kijana huyo aliwahi kutamka kuwa atainywa damu ya wazazi wake, lakini maneno hayo yalipuuzwa.
Majirani
walipofika baada ya kusikia kelele ya marehemu Julitha na kushuhudia
kilichotokea, walimshambulia Gift, wakamponda kichwa na kumwua papo.
via Ritha Chuwalo/WAPO Radio FM.
No comments:
Post a Comment