Monday, February 25, 2013

TALISS SWIM CLUB YAITAKA SERIKALI KUAMKA NA KUJENGA MABWAWA YA KUOGELEA YA UMMA YENYE VIWANGO.



Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa hapa nchini yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).

Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano.

Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.

Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
 
Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
Pichani juu na chini ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar.
 
Picha juu na chini Sehemu ya watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
 
Picha juu na chini Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiwavalisha medali washindi wa mashindano hayo katika kategori mbalimbali. CFAO Motors imeamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuona umuhimu wa vijana kujua kuogelea ili kuweza kujiokoa katika majanga yanayohusiha ajali za majini zinazopelekea vifo vya watoto ikiwa ndio lengo la TALISS.
Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed akikabidhi medali kwa mmoja wa washindi wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne Mcintosh ambaye pia alikuwa MC katika mashindano hayo akikabidhi vikombe kwa washindi wa jumla walioshiriki TALISS Swimming Championships 2013.
 
 
Umati wa watu wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa pamoja makocha waliohudhuria kushuhudia mashindano ya kuogelea ya TALISS yaliyohusisha vilabu kutoka sehemu mbalimbali.
Pichani juu na chini baadhi ya wageni waliohudhuria kutazama mashindano ya kuogelea katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) wakikagua gari mpya aina ya Nissan Y62 inayosambazwa na Kampuni ya CFAO Motors.

No comments:

Post a Comment