BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA TAMKO HILO
TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKOA WA MBEYA
TAMKO
RASMI KUTOKA KTK JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA
MHESHIMIWA
NDG. ABAS KANDORO,
KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE
YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).
NDUGU MKUU WA MKOA,
“HAKI
HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE” (Mit. 14:34).
Katika
mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013
Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea
kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO
NA UISLAMU.
Jukwaa hilo
lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo)
Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian
Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT).Mbali na
mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya
tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na
kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas
tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya
tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama
isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa
amani na uthabiti (Stability) wan chi.
Katika
kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo
yanayotendeka waziwazi yenye athri kubwa kwa amani na usitawi wan chi na wanchi
wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi
unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari
vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli
zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za
ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali
kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua
harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.
Miongoni mwa
harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga,
kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani
Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na
sasa kifo
Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule
Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa
kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya
wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua
zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi
wapenda amani. Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa
wanchi wenzetu moja ni ile ya wenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John
Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa
kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi
kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo
madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na
badala yake Serikali inakaa kimya au ina chukua hatua ambazo kimsingi hazitatui
tatizo ili wananchi waridhike na Seeikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia
haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo
jitokeza kule Mwanza waziri wan chi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu
mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA
SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha
waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu
inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa
na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa
sheria.
Kupigwa
risasi kwa Pdri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha hazma halamu na batili
ya “Ua, chinja” mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi
iliyohasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini
pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya
serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi ziana
muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa. Pamoja na
mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia
mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wan chi. Utasikia mala ikisema “Mtu
haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi” na ndipo kikundi Fulani kitaibuaka na
kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali
hiyohiyo ikitowa kauli kwamba “Mvumiliane” je tunakwenda wapi?
Kwa misingi
hiyo kwanini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM)
inaibeba dini ya kiislamu? Kwakuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni
kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao
na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama
raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya
kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.
HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe
imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo ya fuatayo ni lazima
yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:
- Tunataka Serikali izingatie utawala washeria
kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio
vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi
kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4) na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa
sheria.
- Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya
kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua
inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwakuwa wote wako sawa mbele
ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika
swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua
zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na
mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya
msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama
katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi,
kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na
vifungu vyake viwili vidogo.
- Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gain
zaidi inayoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na
Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala utawala wa sheria.
- Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi
kauli ya waziri wan chi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa
waislamu kama inatokana na sheria gain ya nchi?
- Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria,
tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.
- Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi
katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongovi wa dini ya kikristo
tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha
mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.
Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa
Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa
wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani
ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya
lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.
Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe
6/12/2012.
NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.
Nakala kwa:
- Mwenyekiti
wa CCM Mkoa.
- Tanzania
Christian Furum Taifa
- Mwenyekiti
wa the Tanganyika Law Society.
- Vyombo
vya habari TV, Redio na magazeti
PICHA NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment