Monday, May 20, 2013

BIASHARA YA UKAHABA YASHAMIRI DODOMA,MAKAHABA WA DAR NAO WAPIGA KAMBI HUKO KATIKA KIPINDI HIKI CHA BUNGE...!!

BIASHARA ya ngono katika mji wa Dodoma imeshika kasi kubwa ambapo imebainika kuwa wateja wakubwa ni watumishi wa serikali, wanasiasa na madereva.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa katika biashara hiyo kuna makundi mbalimbali yanayotofautiana kwa malipo ya biashara hiyo.

Wapo wanafunzi wa vyuo vikuu na wanawake ambao wamedai kuwa wanalazimika kufanya biashara hiyo kutokana na kubanwa na maisha, hususani katika marejesho ya mikopo wanaichukua kutoka katika taasisi mbalimbali ya kifedha.

Mmoja wa wafanyabiashara ya ngono (jina tunalo) bila kujua anaongea na nani, alieleza kuwa kwa sasa katika mji wa Dodoma kuna ushindani mkubwa wa biashara ya ngono kwani wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini hapa vimeteka soko hilo.

Alisema kutokana na ushindani huo kwa sasa kima cha chini ni sh 7,000 kwa mchepuo mmoja na sh 30,000 hadi 40,000 kwa kulala.

Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa wateja wakubwa wa ngono ni wafanyakazi wa serikali, wanasiasa (wabunge), madereva pamoja na wafanyakazi wa benki.



Bila hofu mfanyabiashara huyo alieleza kuwa kuanzia muda wa saa tatu hadi sita usiku wanajipanga katika maeneo ya biashara na yanapofika magari hujipanga mbele ya gari ili mteja amchague anayemtaka.

“Hapa tupo wengi, lakini pia wengine ni wafanyakazi wa serikali wanakuja hapa kujiuza, wanafunzi wa vyuo vikuu nao hivyo hivyo… Mimi nipo hapa ninakuja kwa siku maalum ambazo ninakuwa nimekwama.

“Ninakabiliwa na masuala ya mikopo. Unajua hapa tupo kama kumi akina mama ambao tumekopa mikopo katika taasisi mbalimbali, lakini mitaji inapoyumba unajiuliza utapata wapi, unalazimika kuja kufanya biashara,” alisema.

Aliongeza kuwa kwa kawaida mtu mmoja anaweza kufanya ngono na watu wasiopungua saba kwa siku, hivyo ana uhakika wa kujipatia kiasi cha sh 70,000 iwapo siku itakuwa nzuri.

Alibainisha kuwa na kama siku ni mbaya anaweza kupata kiasi cha sh 49,000 iwapo atalipwa sh 7,000 kwa mchepuo mmoja.Uchunguzi wa kina uliofanyika umebaini maeneo ambayo yana wasichana wengi ambao ni makahaba ni Chako Nichako, Double H na Mtaa wa Uhindini ambako kuna gesti maarufu kwa kufanya biashara hiyo.

Hata hivyo, imebainika kuwa makahaba wa vyuo vikuu viwango vyao ni kuanzia sh 200,000 kulala na sh 30,000 kwa mchepuo mmoja.

Mmoja wa waendesha bodaboda ambaye hakutaka jina lake litajwe, alieleza kuwa katika biashara hiyo yapo maeneo ambayo kwa sasa kuna wakala wenye kundi kubwa la wasichana anaowauza.

Wakati biashara ya ngono ikionekana kushamiri, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi alishatangaza kuwawinda na kuwatia kwenye mikono ya sheria wale wanaojihusisha nayo.

Hata hivyo, kauli hiyo inaonekana kukosa mashiko kwani biashara hiyo inazidi kushamiri siku hadi siku.

Imeandikwa na

Danson Kaijage, Dodoma

No comments:

Post a Comment