Monday, May 20, 2013

HIVI NDIVYO WANAJANGWANI WALIVYOMLAKI KIPENZI CHAO MRISHO NGASSA..!

Ngassa amezungumza kwa mara ya kwanza na kuthibitisha kwamba kweli amesaini Yanga.
“Ni kweli nimesaini Yanga, nisingeweza kuzungumzia suala hilo wakati nina mkataba ambao ulikuwa haujamalizika.
“Lakini baada ya mechi ya mwisho ya ligi, sasa niko huru kuanza kuutumikia mkataba wangu mpya,” alisema.
Mashabiki wa Yanga walimchukua Ngassa na kumvisha jezi ya njano na kijani, mara tu baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Yanga na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, jana.
Mashabiki hao walimvisha jezi hiyo na kumbeba na kumbeba na kuondoka naye hadi nje ya uwanja.
Azam FC ilimpeleka Simba kwa mkopo, lakini Simba imekuwa ikisema ilimuongezea mkataba wa mwaka mmoja na kumlipa Sh milioni 30 pamoja na gari.


Kama unahitaji picha ambazo alikuwa akisani mkataba huo mpya wa Yanga ingia hapa www.facebook.com/edwintanzania

No comments:

Post a Comment